English

Idar-Oberstein, Ujerumani

Nilipata pia nafasi ya kutembelea kiwanda cha kihistoria cha ukataji wa madini ya vito. Kiwanda hicho kilikuwepo kabla ya umeme kuanza kutumika. Hadi leo hii kinaendelea kutumika kwa kutumia nguvu ya maji moja kwa moja. Vile vile gurudumu linalosukumwa kwa maji hutumika kuwashia jenereta dogo kwa ajili ya taa ndani ya kiwanda hicho.





















Nilifurahi sana kutembelea eneo hili la kihistoria na kujua ni jinsi gani walivyofanikiwa kukata na kung'arisha madini ya vito kabla ya ugunduzi wa umeme. Kuona bwawa dogo na gurudumu nililokuwa likisukumwa kwa maji. Na kuzalisha umeme uliokuwa ukitumika kiwandani hapo. Mji wa Idar-Oberstein ulianzisha na kuendeleza kiwanda cha ukataji wa madini kutokana na kuwepo kwa madini ya agate katika eneo hilo.



Kozi
Vifaa
Matukio yajayo
Madini & migodi
Kazi zangu
Sifa zangu
Mawasiliano
Mwanzo   Notisi ya faragha
logo

© Hati miliki ya picha zote Noreen Masaki